Agizo la RTO Arusha kwa Mabasi ya abiria laanza kutekelezwa, Atoa onyo kwa Wamiliki wa Malori
Na Gasto Kwirini wa Jeshi la Polisi Arusha Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa operesheni ya ukaguzi wa magari Mkoani Arusha, leo tarehe 11.07.2019 muda wa asubuhi imebainika baadhi ya Wamiliki, Madereva na Makondakta wameanza kuitikia wito wa kutozidisha abiria katika mabasi yao na kufuata sheria bila kushurutishwa. Operesheni hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP)Joseph Bukombe imeanza kuonyesha matokeo chanya baada ya ukaguzi kufanyika katika Mabasi yanayofanya safari zake kati ya Arusha na Kiteto, ambapo hayakuzidisha abiria kama ilivyozoeleka kwa mabasi mengi yanayopita njia hiyo. Akitolea mfano Basi la Kampuni ya Mtei Express, Mkuu huyo wa Usalama barabarani ameipongeza kampuni hiyo, dereva pamoja na Kondakta kwa kuitikia wito wake alioutoa kwa wamiliki, madereva na Makondakta kwa kuhakikisha wanafuata Sheria za usalama barabarani, ambapo mabasi mengi yalikua yanajaza Abiria kuliko uwezo